Kuna mahusiano yepi kati ya swalah na matamanio?

Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ

“Wakafuata baada yao waovu walipoteza swalah na wakafuata matamanio.”[1]

Kuna mafungano yepi kati ya kupoteza swalah na kufuata matamanio?

Jibu: Kwa sababu swalah inakataza machafu na maovu. Kwa hiyo unapoipoteza basi unafuata matamanio. Mtu huyu hana swalah inayomkataza machafu na maovu.

[1] 19:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/03/2023