05. Dalili ya nne juu ya kufaradhishwa kufunga Ramadhaan

4 – Hadiyth ya Jibriyl refu[1] inayojulikana aliyoipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh). Vilevile ameipokea al-Bukhaariy kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kwa kifupi[2] ambapo Jibriyl alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Uislamu, imani, ihsaan na Saa. Wakati alipomuuliza ni nini Uislamu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijibu:

“Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba kwa atakayeweza kuiendea… “

[1] Muslim (08).

[2] al-Bukhaariy (50).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ilmaam bishay´ min Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 27/03/2023