Muda wa chini kabisa wa I´tikaaf

Swali: Ni upi muda wa chini kabisa wa kukaa I´tikaaf?

Jibu: Hakuna kikomo cha muda uliopangwa. I´tikaaf haina muda wa chini kabisa wala wa juu kabisa. Ni jambo halikupokelewa katika Shari´ah kuweka kikomo cha muda.

Swali: Wako wanaosema kuwa ni saa moja?

Jibu: Ni jambo halina dalili. Katika muda hakuna chini ya saa moja? Jambo hilo ni kwa njia ya kupigia mfano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21930/ما-اقل-وقت-للاعتكاف
  • Imechapishwa: 14/01/2023