Swali: Vipi kwa mwenye kutaka kulipa I´tikaaf katika Shawwaal?

Jibu: Hapana vibaya. Ni jambo limefanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikimkuia wepesi na akapenda kufanya I´tikaaf, ijapo sio laizma. Ni jambo linalopendeza.

Swali: Maalik amesema:

“Huku kwetu katika watu wa al-Madiynah hakuna anayetambulika kwa I´tikaaf isipokuwa Muhammad bin Abiy Bakr na mwingine mmoja.”

Jibu: Maalik ni mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni. Hata hivyo sio hoja. Hoja ni kwa yale yaliyosemwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21931/هل-يجوز-قضاء-الاعتكاف-في-شوال
  • Imechapishwa: 14/01/2023