Ni kujifananisha na tabia za kike

Swali: Kuna mahusiano yoyote kati ya kunyoa ndevu na kujifananisha na tabia za kike?

Jibu: Ni haramu. Ndani yake kuna kujifananisha na wanawake. Kwa sababu wanawake ndio wasiokuwa na ndevu.

Swali: Lakini baadhi ya wanazuoni wanamwingiza mnyoa ndevu katika hukumu ya mwenye kujifananisha na tabia za kike?

Jibu: Amelisimulia Ibn ´Abdil-Barr kutoka kwa baadhi ya wanazuoni. Kwa sababu kuwepo kwa ndevu pasi na nywele kuna kujifananisha na wanawake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21932/هل-يعد-حلق-اللحية-من-التخنث
  • Imechapishwa: 14/01/2023