Mtume hakhusishiwi ´ibaadah hata moja hata kama ni mbora kuliko Ka´bah

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni jambo linalojulikana kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni bora kuliko Ka´bah. Lau wangelijua kuwa makusudio ya hayo [kuzuru maiti wa Kiislamu] ni kumuabudu Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, kumuomba Yeye na du´aa, vivyo hivyo makusudio ya kutembelea kaburi [lake] ni kwa ajili ya kuliombea du´aa, kama jinsi anavyomkusudia kwa kumswalia maiti, basi hili lingeondoka kwenye nyoyo zao.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kiumbe bora. Ka´bah ni kiumbe pia katika viumbe. Kiumbe bora pasina kipingamizi ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini Ka´bah ni mahala pa ´ibaadah; ni mahala pa Twawaaf, swalah, I´tikaaf na kadhalika. Zote hizi ni ´ibaadah anafanyiwa Allaah (´Azza wa Jall). Ka´bah ndio mahala pa kukhusishwa na ´ibaadah. Ama kuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume anayefikisha Da´wah, ametimiza amana, ameunasihi Ummah na amepigana Jihaad kwa Allaah ukweli wa kupigana. Ka´bah ina umuhimu wake na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na umuhimu wake mwengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatakiwa kutukuza, kupendwa, kufuatwa na kutiiwa. Kwa kuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Ka´bah inaendewa, kunaswaliwa hapo na inaelekewa [Qiblah] kwa kuwa ni Nyumba ya Allaah. Ka´bah ni mahala pa ´ibaadah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye amefikisha ´ibaadah hii na akawabainishia nayo watu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2247
  • Imechapishwa: 05/05/2015