Waabudia makaburi wameyapindua mambo

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Hata miongoni mwao [waabudia makaburi na washirikina] wanaitakidi kuwa kutembelea majumba yaliyo kwenye makaburi, ima kaburi la Mtume, Shaykh au baadhi ya watu wa kwa nyumba ya Mtume, ni bora kuliko kwenda kuhiji Masjid-ul-Haraam. Matembezi hayo wanaitwa kuwa ni Hajj kubwa.”

Baadhi yao wanafadhilisha kuyatembelea zaidi kuliko hata Hajj ambayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu na ambayo Allaah (Ta´ala) amesema juu yake:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا

“Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea.” (03:97)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameihesabu Hajj kuwa ni katika Jihaad katika njia ya Allaah kutokana na fadhila zake kubwa, juhudi, mali na tabu. Ni aina ya Jihaad. Hakuna kitu kilicho bora kuliko Hajj isipokuwa yaliyoitangulia hiyo Hajj katika faradhi za Kiislamu, Tawhiyd, swalah, zakaah na swawm ya Ramadhaan. Hajj sio bora zaidi kuliko zingine, bali ni miongoni mwa ´ibaadah bora na matendo mema. Lakini watu hawa [waabudia makaburi] wameyapindua mambo na kusema kuwa kuyatembelea majumba [makuba] na makaburi ni bora kuliko kwenda kuhiji Nyumba ya Allaah tukufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2247
  • Imechapishwa: 05/05/2015