Chukua mfano wa dawa. Kwa mfano mtu anaweza kujitibu kwa kitu cha haramu na akapona. Je, hii ni dalili inayoonesha usahihi wa kujitibu kwa vitu vya haramu? Hapana. Haitolei dalili ya hilo. Lakini kupatikana athari hii sio dalili ya usahihi wa njia ambayo mtu anatakiwa kutumia katika kujitibu. Bali Allaah anaweza hata kumponya [kupitia haramu hiyo]. Lakini aliyokhasirika nayo katika dini yake na ´Aqiydah yake ni mambo makubwa zaidi kuliko hayo lau angeliendelea na hayo maradhi.

Kwa mfano yule anayejitibu kwa uchawi. Uchawi ni kufuru na ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Tuchukulie kuwa amejitibu kwa mchawi na akapona na uchawi aliokuwa nao, hata hivyo ´Aqiydah yake imeharibika na ameiuza dini yake – tunaomba kinga kwa Allaah. Ni lipi ambalo ni kheri? Lau angelisubiri kwa maradhi yake hata kama hiyo itapelekea kufa kwa maradhi haya ilihali ni mwenye kushikamana bara bara na dini yake na yuko thabiti katika ´Aqiydah yake, ni lipi ambalo ni kheri, ikiwa atakufa ilihali ni kafiri na ni mwenye kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall)? Mtu atazame matokeo na alinganishe baina ya manufaa na madhara. Asifanye mambo pasina kufikiria na kuzingatia. Kwa ajili hii ndio maana Allaah Ametuharamishia kujitibu kwa mambo ya haramu. Ametuharamishia kujitibu kwa uchawi. Ametuharamishia kujitibu kwa uchawi na talasimu na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1429-12-1.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015