Tofauti ya kufanya Tabarruk mahala alipokusudia Mtume na ambapo hakukusudia

Hii ndio tofauti kati ya yenye kujuzu – Tabarruk – na isiyojuzu. Mahala penye kujuzu ni pale alipokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali mahala hapo. Anatakiwa kuigwa baada ya hapo. Hili halina ubaya wowote. Ama isiyojuzu ni zile sehemu ambapo hakukusudia kupaswalia, bali alifanya hivyo kwa sababu ya haja fulani tu. Sehemu kama hizi hatakiwi kuigwa baada ya hapo. Mfano wa sehemu ya kwanza ni kama alivofanya ´Utbaan (Radhiya Alllaahu ´anh). Alikuwa ameazimia kufanya mahala pa kuswalia (Muswallaa) nyumbani kwake wakati ambapo atashindwa kwenda msikitini. Alitaka mtu wa kwanza kupaswalia awe ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio makusudio. Mtume alikusudia hilo ili kutekeleza matakwa ya ´Utbaan bin Maalik na Mtume alikusudia kuswali mahala hapo. Hakuna neno kumuiga kwa kuswali sehemu kama hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivyo kwa ajili ya makusudio haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1429-11-10.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015