Mswaliji amesahau akasimama Rak´ah ya tatu katika Tarawiyh II

Swali: Vipi ikiwa mswaliji atasimama kwa Rak´ah ya tatu kwa kusahau?

Jibu: Arudi; kwa sababu swalah ya usiku ni Rak´ah mbilimbili. Arejee na atatakiwa kusujudu sijda ya kusahau. Hili ni sawa na hali ambapo mtu atasimama katika Rak´ah ya tatu kwa kusahau katika Fajr au ijumaa, anapaswa pia kurudi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24878/حكم-القيام-لثالثة-في-التراويح-ساهيا
  • Imechapishwa: 26/12/2024