Swali: Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa ni za Sunnah?

Jibu: Hizo ni za Sunnah ya Raatibah, Raatibah ya ´Ishaa. Ama kuhusu Witr inakuja baada ya hapo. Anaweza kuswali Rak´ah mbili kisha akaongeza Rak´ah moja kwa ajili ya Witr, au hapana vibaya anaweza kuswali pia Rak´ah moja tu. Ikiwa ataswali Rak´ah moja tu baada ya Rak´ah za Raatibah, tayari atakuwa amekamilisha Witr yake. Na ikiwa ataongeza, kama vile kuswali Rak´ah tatu, tano au zaidi, basi atapata thawabu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24872/هل-الركعتان-بعد-العشاء-هما-السنة-الراتبة
  • Imechapishwa: 26/12/2024