Ibn Baaz kuhusu ulazima wa mswaliji kuweka Sutrah mbele yake

Swali: Kuhusu Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ya pili aliposema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali bila ya kuelekea kwenye ukuta.”

Jibu: Baadhi yao wameitumia kama dalili ya kwamba hakuna haja ya kuwa na Sutrah, lakini hata hivyo si yenye uwazi wa moja kwa moja, kwa sababu imekanusha kutokuwepo kwa ukuta tu na haikanushi uwepo wa Sutrah. Kwa hivyo inawezekana kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali huku akiwa na Sutrah kama kijiti cha anaza mbele yake. Kwa hivyo kutokuwepo kwa ukuta hakumaanishi kutokuwepo kwa Sutrah, kama ilivyoelezwa awali.

Swali: Je, kuna dalili wazi kutoka kwa wanazuoni wanaosema Sutrah si lazima?

Jibu: Sijui. Kuna Hadiyth ya Ibn ´Abbaas, lakini ina mtuhumiwa ambaye al-Hajjaaj bin Artwaa’ah, kama ilivyotangulia.

Swali: Ikiwa imamu hakuweka Sutrah na punda akapita mbele ya baadhi ya safu za waumini?

Jibu: Hilo halidhuru. Jukumu liko kwa imamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24870/حكم-السترة-والمرور-امام-المصلي
  • Imechapishwa: 26/12/2024