Ibn Baaz kuhusu mwanamke kukata swalah Madiynah na wa Makkah

Swali: Je, mwanamke hukata swalah?

Jibu: Hapana, katika msikiti wa Madiynah na wa Makkah kunasamehewa kutokana na dharurah:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Kwa sababu hiyo kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba swalah haikatiki katika msikiti wa Madiynah na wa Makkah kutokana na msongamano.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24868/هل-تقطع-المراة-الصلاة-في-الحرمين
  • Imechapishwa: 26/12/2024