Msafiri wa mara kwa mara katika Ramadhaan

Swali: Mimi ni mtu mwenye safari endelevu mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta riziki na daima hukusanya swalah za faradhi safarini na hula katika mwezi wa Ramadhaan. Je, nina haki ya kufanya hivo au hapana?

Jibu: Inafaa katika safari yako kufupisha zile swalah za Rak´ah nne na kukusanya Dhuhr na ´Aswr katika wakati wa swalah moja wapo na kukusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa katika wakati wa swalah moja wapo. Aidha inafaa kwako kula katika mwezi wa Ramadhaan unapokuwa katika safari yako. Ni lazima kwako kulipa zile siku za Ramadhaan ulizokula. Amesema (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.” (02:185)

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/213) nr. (8324)
  • Imechapishwa: 26/04/2022