Miaka 60 haujui kuwa anatakiwa kulipa siku alizoacha kufunga wakati wa swawm

Swali: Kuna kikongwe mwenye miaka sitini na alikuwa hajui hukumu za hedhi kwa miaka mingi kipindi alipokuwa anapata hedhi. Hakulipa swawm ya Ramadhaan kwa kudhani kuwa hailipwi kutokana na yale aliyoyasikia kutoka katika vinywa vya watu.

Jibu: Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah kutokana na hilo kwa sababu hakuwauliza wanazuoni. Sambamba na hilo ni lazima kwake kulipa idadi ya zile siku alizoacha kwa mujibu wa vile dhana yake kubwa inavompelekea na kutoa kafara kwa kumlisha masikini chakula kwa kila siku aliyoacha nusu pishi ya ngano, tende, mchele au mfano wake katika kile chakula kinacholiwa kwa wingi katika mji akiwa anaweza kulisha chakula. Akiwa hana uwezo wa kulisha chakula basi hatohitajia na itamtosha kulipa funga.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/152) nr. (1790)
  • Imechapishwa: 26/04/2022