Swawm ya anayeona umanjano baada ya kusafika

Swali: Nina shangazi ambaye amesafika ndani ya Ramadhaan kabla ya kupambazuka alfajiri ambapo akafunga siku hiyo. Alipotaka kuswali Dhuhr akaona umanjano. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Ikiwa amesafika kabla ya kuingia alfajiri kisha akafunga basi swawm yake ni sahihi na ule umanjano hauathiri baada ya kuona usafi. ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na maji ya uchafuchafu kuwa ni kitu baada ya kusafika.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (13507)
  • Imechapishwa: 26/04/2022