Swali: Kuna baadhi ya wamiliki wa malori na wale wanaofanya kazi hiyo mwaka mzima wanakuwa safari. Je, inafaa kwao kula ndani ya Ramadhaan? Ni wakati gani wanatakiwa kulipa?

Jibu: Ikiwa ule umbali wanaosafiri ni umbali ambao unakubalika kufupisha swalah basi imesuniwa kwao kula katika safari yao. Ni lazima kwao kulipa zile siku za mwezi wa Ramadhaan walizokula kabla ya kuingia Ramadhaan inayofuata. Amesema (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.” (02:185)

Inawabidi wachague zile siku watazolipa ndani yake  masiku waliyokula katika masiku ya Ramadhaan kwa ajili ya kukusanya kati ya kuwaondoshea uzito na kulipa yale masiku ya funga wanayodaiwa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (6281)
  • Imechapishwa: 26/04/2022