Msafiri anapaswa kukamilisha swalah ikiwa hahisi uzito?

Swali: Je, imepokelewa kwa Salaf kukamilisha swalah safarini na kusema kwamba uzito umekwishaondoka?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba alikuwa akifupisha safarini na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkubalia.  Imekuja katika upokezi mwingine ya kwamba aliyafanya baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imekuja katika upokezi ya kwamba alimkubalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini kilichothibiti kutoka kwake ni kwamba amesema:

“Sipati ugumu.”

Alikuwa akiswali Rak´ah nne na akisema:

“Sipati ugumu.”

Hivi ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni, kwa sababu kufupisha swalah kunapendeza na sio jambo la lazima. Ni kama ambavo mtu anapokuwa safarini katika Ramadhaan kula ndio bora ingawa inafaa pia kufunga.

Swali: Ugumu ukimalizika aswali kwa kukakamilisha?

Jibu: Hapana. Inapendeza kwa msafiri kufupisha katika hali zote hata kama amepumzika. Msafiri anatakiwa kuswali Rak´ah mbilimbili. Hata hivyo hapana neno ikiwa ataswali kwa kukamilisha. ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na Maswahabah wengine walikuwa wakiswali kwa kukamilisha katika hijjah zao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23060/هل-يتم-المسافر-الصلاة-لو-زالت-المشقة
  • Imechapishwa: 24/10/2023