57. Ni wafalme wangapi Mtume aliwatumia ujumbe mwaka wa 6?

Swali 56: Ni wafalme wangapi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatumia ujumbe?

Jibu: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma Dihyah bin Khaliyfah kwenda kwa Qayswara mfalme wa kirumi, ´Abdullaah bin Hudhaafah as-Sahmiy kwenda kwa Kisraa mfalme wa kifursi, ´Amr bin Umayyah adh-Dhwimriy kwenda an-Najaashiy mfalme wa Uhabeshi, Haatwib bin Abiy Balt´ah till Muqawqi kwenda kwa mfalme wa Alexandria, ´Amr bin al-´Aasw kwenda kwa Jayfar bin al-Julandiy na ´Abd bin al-Julandiy anayetokana na Azd  kwenda Oman, Sulaytw bin ´Amr kwa Thumaamah bin Athaal na Huudhah bin ´Aliy anayetoka Banuu Haniyfah kwenda Yamaamah, al-´Alaa’ bin al-Hadhwramiy kwenda kwa al-Mundhir bin Saawaa al-´Abdiy mfalme wa Bahrain na Shuja´ bin Wahb al-Asdiy kwenda kwa al-Haarith bin Abiys-Shamr al-Ghassaaniy mfalme wa pande za Shaam. Imesemekana vilevile kwamba alitumwa kwenda kwa Jabalah bin al-Ayham al-Ghassaaniy. Alimtuma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia al-Muhaajir bin Abiy Umayyah al-Makhzuumiy kwenda kwa al-Haarith bin ´Abd Kulaal al-Humayriy. Kwa mujibu wa wanahistoria hayo yalitokea katika Dhul-Hijjah na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 119-120
  • Imechapishwa: 22/10/2023