Ni lini msafiri analazimika kuswali msikitini?

Swali: Inafaa kwa mtu aliyesafiri peke yake kufupisha swalah licha ya kwamba anaishi pembezoni na msikiti?

Jibu: Hapana, aswali Rak´ah nne na wengine. Yuko peke yake na hana ndugu mwingine pamoja naye?

Muulizaji: Hapana.

Ibn Baaz: Akipata mkusanyiko basi inamlazimu kuswali na mkusanyiko.

Swali: Vipi kuhusu ruhusa ya safari?

Jibu: Ndio, lakini hilo ni pale ambapo mtu anakuwa hana mkusanyiko. Lakini akiwa na mkusanyiko basi ataswali na mkusanyiko, kwa sababu mkusanyiko ni lazima na kufupisha swalah kunapendeza. Haijuzu kuacha jambo la lazima kwa ajili ya jambo linalopendeza.

Swali: Akifupisha swalah peke yake anapata dhambi kwa sababu kuna msikiti karibu naye?

Jibu: Anapata dhambi, kwa sababu ameacha swalah ya mkusanyiko. Swalah ya mkusanyiko ni lazima. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kusikia wito na asiuitikie, basi hana swalah isipokuwa kwa udhuru.”

Isitoshe alimwamrisha kipofu kuswali pamoja na wengine hata kama hana wa kumwongoza njia. Alimjibu:

“Inakulazimu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23059/متى-تلزم-المسافر-صلاة-الجماعة
  • Imechapishwa: 22/10/2023