Aombe du´aa ndani au nje ya swalah?

Swali: Bora kuomba du´aa ndani ya swalah inayopendeza au baada ya kumaliza kuswali?

Jibu: Bora ni kuomba katika Sujuud. Bora ni katika Sujuud na mwishoni mwa swalah kabla hajatoa salamu. Simaanishi baada ya kumalizika swalah, kabla hajatoa salamu. Hivi ndio bora na karibu zaidi kuitikiwa du´aa. Vivyo hivyo katika hali ya Sujuud. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa amesujudu. Hivyo basi ombeni du´aa kwa wingi.”

“Ama Rukuu´ mtukuzeni Mola. Ama Sujuud jitahidini katika du´aa kuna matarajio mkubwa mkaitikiwa.”

Bi maana kuna uwezekano mkubwa zaidi wa nyinyi kuitikiwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anapomaliza mmoja wenu Tashahhud ya mwisho, basi aombe kinga dhidi ya mambo manne.”

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakapomaliza Tashahhud basi achague ile du´aa inayompendeza zaidi kisha aombe kwayo.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23033/ما-المواضع-الافضل-للدعاء-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 22/10/2023