92. Tofauti ya nguo za wanamme na nguo za wanawake

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kinachopambanua kati ya mavazi ya wanamme na mavazi ya wanawake kunatokana na yale yanayofaa kwa wanamme na yale yanayofaa kwa wanawake ambapo kila mmoja katika wao ataamrishwa mavazi hayo. Wanawake wameamrishwa kujistiri. Hawatakiwi kuonyesha mapambo na ya kuvutia. Kwa ajili hiyo ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kwao kunyanyua sauti katika kutoa adhaana, wakati wa hajj na wakati wa kupanda Swafaa na Marwah. Wala wanawake hawatakiwi wakati wa hajj kuvaa kama wanavyovaa wanaume. Kwa mfano wanamme wameamrishwa kufunika vichwa vyao na wasivae mavazi yaliyozoeleka na mavazi yaliyoshonwa, kama vile shati, suruwali, burnus wala soksi za ngozi. Lakini wakati mwanaume anapokuwa anahitaji kitu cha kufunika uchi wake na kutembea kwacho na asipate shuka ya chini na makubadhi, basi akaruhusiwa kuvaa suruwali na soksi za ngozi kutokana na haja yenye kuenea. Hilo ni tofauti na ile haja maalum, kama vile maradhi au baridi, atalazimika kutoa fidia. Kwa ajili hiyo Abu Haniyfah ameraddi kipimo hiki. Wanazuoni wengi hawakuafikiani naye kutokana na ile Hadiyth Swahiyh[1] na kuwepo tofauti kati ya hayo mawili. Kuhusu mwanamke hakuamrishwa kubadilisha chochote katika mavazi yake kwa sababu yeye ameamrishwa kujisitiri. Hata hivyo amekatazwa kuvaa Niqaab na vifuniko vya mikono kwa sababu hayo ni mavazi yaliyoshonwa na hayahitajiki.”[2]

[1] Bi maana maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muhrim asivae kanzu, kilemba, suruwali, burnus wala soksi isipokuwa ikiwa kama hakupata ndala. Katika hali hiyo avae soksi za ngozi na azikate chini ya kongo mbili za miguu. Asivae nguo yoyote iliyopakwa Was (mti wa umanjano) wala zafarani.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Upokezi ni wa al-Bukhaariy na ipo katika ”al-Irwaa´” (1012). Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Udhahiri ni kwamba ambaye hakupata ndala na hivyo akavaa soksi za ngozi hahitaji kutoa fidia. Wameraddiwa kwa hoja kwamba fidia ingelikuwa ni wajibu basi angelibainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ilikuwa kipindi cha haja.” (Fath-ul-Baariy)

Hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitoa Khutbah ´Arafah:

”Yule asiyepata shuka ya chini basi avae suruwali, na yule asiyepata ndala basi avae soksi za ngozi.” (Irwaa’-ul-Ghaliyl (1013))

[2] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 22/10/2023