91. Mavazi ya mwanamke katika miji ya baridi

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Isitoshe haya hayahusu sitara peke yake. Endapo mwanamke atavaa suruwali au soksi pana na imara za ngozi kisha akaweka juu yake jilbaab kwa kiasi cha kwamba hayaonekani maumbo yake, basi lengo litakuwa limefikiwa. Soki za ngozi laini zinazoonyesha maumbo ya nyayo ni za wanamme. Vivyo hivyo endapo mwanamke atavaa kanzu na manyoya kwa sababu anahitaji kujikinga na baridi; hatokatazwa kutokana nayo. Endapo mtu atasema kuwa hapo kitambo wanawake hawakuwa wakivaa manyoya, jibu ni kwamba hilo limefungamana na haja. Nchi za baridi zinahitaji mavazi mazito na yenye kutia joto ingawa mtu hayahitaji katika nchi zenye joto.”[1]

[1] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 153
  • Imechapishwa: 22/10/2023