Kulipa Dhikr za baada ya swalah

Swali: Endapo mtu atasahau Dhikr baada ya kumalizika swalah:

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

kwa sababu ya kughafilika na akakumbuka baada ya kitambo azisome baada ya kuondoka katika swalah kwa kitambo fulani?

Jibu: Azidiriki kwa njia ya kufanya Dhikr kwa wingi. Vinginevyo ni Sunnah iliyopita nafasi yake. Azidiriki kwa njia ya kumtaja Allaah (´Azza wa Jall), kwa hakuna wakati maalum wa kumtaja Allaah. Ndani ya mchana na usiku wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23065/هل-يشرع-قضاء-اذكار-الصلاة-بعدها-بمدة
  • Imechapishwa: 24/10/2023