56. Ni misafara gani ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 6?

Swali 56: Ni misafara gani ya kijeshi ilifanyika mwaka huo?

Jibu: Msafara wa kijeshi wa Abu ´Ubaydah kwenda kwa Dhul-Qasswah na msafara wa kijeshi wa Zayd bin al-Haarithah kwenda Banuu Sulaym pamoja na misafara yake ya kijeshi kwenda Banuu Tha’labah na dhidi ya msafara wa Abul-´Aasw huko Jumaadaa al-Uulaa. Kwa hiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimpa ulimzi Abul-´Aasw, kwa vile alikuwa amemuoa msichana wake Zaynab, na akamrudisha na msafara wake.

Katika mwaka huohuo, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf alitumwa katika msafara wa kijeshi hadi Dawmat-ul-Jandal ambapo wakazi wake walisilimu.

Mwaka huo pia ndio kulitokea tukio hilo kwa watu wa ´Uraynah. Walimpiga vita Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), wakamuua mchungaji wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), wakamchukua ngamia kisha baadaye wakakamatwa, wakasulubiwa na wakauawa. Walikuwa wamekatwa mikono na miguu yao pande tofauti na kung’olewa macho yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 24/10/2023