93. Mwanamke aliye katika Ihraam anafunika uso wake

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Wanazuoni wamekinzana kama uso wa mwanamke ni kama kichwa au mwili wa mwanaume, Ahmad na wengine wana maoni mawili juu ya suala hilo. Wale wenye kuona kuwa uso wake ni kama kichwa cha mwanaume wamemwamrisha kufunika uso wake kwa kitambaa pasi na kitambaa hicho kugusa uso, kama ambavyo mwanaume anakota kivuli kichwa chake kwa kitambaa bila ya kitambaa hicho kugusa kichwa chake. Ambaye ameona kichwa chake ni kama mikono ya mwanaume – jambo ambalo ndio sahihi – hakumkataza kufunika uso, bali alichokatazwa ni kutumia Niqaab kama alivyokatazwa kutumia vifuniko vya mikono. Ni kama ambavo mwanaume amekatazwa mashati, suruwali na mfano wake. Hukumu hiyohiyo inatumika juu ya Burqu´ na vilivyotengenezwa kwa lengo la kufunika uso. Ni kama ambavo mwenye kulala anavyofunika kichwa chake kwa mfano wa shuka na mikono miwili kwa mikono ya shati. Hakukatazwa kutokana na mambo hayo.”[1]

[1] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 24/10/2023