Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kwa hiyo ikiwa mwanaume atataka kuvaa Niqaab na Burqu´ na wanawake wakataka kufunua nyuso zao, basi wangekatazwa kutokana na hayo. Kadhalika mwanamke ameamrishwa kuswali kwa kujikusanya na asijiachie viungo vyake[1]. Hayo yakafahamisha kuwa Shari´ah imemwamrisha mwanamke kujisitiri kwa njia ambayo hakuamrishwa mwanamme. Hiyo ni haki ya Allaah juu yake ingawa hakuna yeyote atakayemuona. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Na tulizeni majumbani mwenu na wala msijishauwe mshauwo wa wanawake majahili wa awali.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokana na misikiti ya Allaah. Hata hivyo nyumba zao ni bora kwao.”[3]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Swalah ya mwanamke katika boudoir kwake ni bora kuliko swalah yake kwenye chumba yake, na swalah yake katika chumba yake ni bora kuliko swalah yake katika nyumba yake, na swalah yake katika nyumba yake ni bora kuliko swalah yake katika msikiti wa eneo lake, na swalah yake katika msikiti wa eneo lake ni bora kuliko swalah yake katika pamoja nami.”[4]

Yote haya ni kutokana na kule kujisitiri na kujifunika.”[5]

[1] Sijui dalili yoyote inayofahamisha jambo hili. Isitoshe yanaraddiwa na kuenea kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Swalini kama mlivyoniona ninaswali.”  (al-Bukhaariy (631))

Rejea hitimisho katika kitabu ”Swifatu Swalaat-in-Nabiy”.

[2] 33:33

[3] Ahmad (2/76) na Abu Daawuud (567). Imesahihishwa na Ibn Khuzaymah (1684) na al-Haakim (755).

[4] Hadiyth ni nzuri na ameipokea Ahmad, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”.

[5] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 155
  • Imechapishwa: 24/10/2023