95. Swalah ya mwanamke nyumbani ni bora kuliko msikitini

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Swalah ya mwanamke katika boudoir kwake ni bora kuliko swalah yake kwenye chumba yake, na swalah yake katika chumba yake ni bora kuliko swalah yake katika nyumba yake, na swalah yake katika nyumba yake ni bora kuliko swalah yake katika msikiti wa eneo lake, na swalah yake katika msikiti wa eneo lake ni bora kuliko swalah yake katika pamoja nami.”[1]

[1] Hadiyth ni nzuri na ameipokea Ahmad, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”. Hadiyth hii ni moja katika dalili zinazoyafanya maalum maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Swalah moja katika msikiti huu ni bora kuliko swalah elfu moja katika misikiti mingine isipokuwa katika msikiti Mtukufu. Swalah moja katika msikiti Mtukufu ni bora kuliko swalah laki moja katika misikiti mingine yote.  (al-Bukhaariy (1190) na Muslim (1394))

Hili linafahamisha kuwa ubora huu ni jambo linawahusu wanaume peke yao pasi na wanawake, na kwamba kule kuswali kwao majumbani mwao ni bora kuliko kuswali katika msikiti wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kutokana na hilo utatambua kuwa kusongamana wanawake katika msikiti wake, na khaswa katika msimu wa hajj, ni miongoni mwa mambo yanayoonyesha ujinga wao juu ya Shari´ah au kudharau kwao maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na khaswa kwa kuzingatia kwamba wengi wao wanachanganyika na wanaume hata katika msongamano mkubwa pale ambapo wanaume wanatoka msikitini. Tunamshtakia Allaah kutokana na uchache wa hayaa na uchache wa wivu wa wanaume wao.

Haya ndio niliyoyasema katika chapa zilizotangulia. Kisha ikanibainikia kuwa hakuna chochote kinachojuzisha umaalum katika suala hili na kwamba maoni ya sawa ni kwamba Hadiyth imekuja ni yenye kuenea na inawahusu wanawake pia. Hata hivyo haina maana kwamba si bora kwao kuswali majumbani mwao kama ambavo ni bora kuswali swalah zinazopendeza majumbani kuliko misikitini. Lakini akiswali katika msikiti mmoja wapo miongoni mwa ile misikiti mitatu anapata ujira wa ubora kutokana na misikiti hiyo na inahusu wanawake pia. Kwa msemo mwingine ni kwamba hakuna haja ya msongamano uliyotajwa kwa hali zote. Kwa ajili hiyo inatakiwa kwa wanawake kuachana na jambo hilo na hivyo yataondoka maharibifu mengi. 

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 24/10/2023