Mke juu ya kitanda cha kujifungua

Swali: Kipindi cha mwisho waume wengi wanalalamika kuwa wake zao wanakataa kufanya jimaa – ni mamoja kuna sababu au pasi na sababu – jambo ambalo limepelekea baadhi ya waume kutumbukia katika haramu. Unawanasihi nini wake? Ni lipi la wajibu juu yao?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake mwanamke hazingatiwi kuwa ameketeleza haki ya Mola Wake mpaka atekeleze haki ya mume wake. Lau kama atamtaka nafsi yake [wafanye jimaa] na yeye mwanamke yuko katika kitanda cha kujifungua basi hatomkatalia.”[1]

Anatakiwa kumwitikia jimaa pasi na kujali hali yake na asilete vijiudhuru. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamume atapomwita mke wake kitandani[2] na asije na akalala hali ya kumghadhibikia, basi Malaika wanamlaani mpaka kupambazuke.”[3]

[1] al-Haakim (4/7325) aliyesema kuwa ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana aye. Tazama “Aadaab-uz-Zifaaf”, uk. 175-177 ya al-Albaaniy.

[2] al-Albaaniy amesema:

“Bi maana kwa ajili ya tendo la ndoa.” (Aadaab-uz-Zifaaf, uk. 175-177)

[3] al-Bukhaariy (3238) na Muslim (1436). Tamko ni la al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
  • Imechapishwa: 25/06/2023