Swali: Je, lugha ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) aliokuwa akizungumza ni lugha ya kiarabu?
Jibu: Sidhanii hivo. Sio lugha ya kiarabu. Wengi katika Mitume waliotangulia sio waarabu. Isipokuwa wale ambao walikuwa katika kiziwa cha kiarabu, kama mfano wa Shu´ayb, Swaalih, Nuuh na Luutw. Hawa walikuwa ni waarabu. Wengine walikuwa wanazungumza lugha isiyokuwa ya kiarabu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-08.mp3
- Imechapishwa: 16/11/2014
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
07. Hakuna yeyote awezaye kuifahamu Qur-aan kwa kutegemea ubobeaji wake wa lugha ya kiarabu peke yake
Kutokana na yaliyotangulia inapata kuwa wazi ya kwamba hakuna nafasi kabisa kwa yeyote yule – pasi na kujali ubobeaji wake katika lugha ya kiarabu na adabu zake – kuifahamu Qur-aan tukufu pasi na kutaka msaada kwa hilo kutoka katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) za kimaneno na…
In "Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam"
Kiarabu lugha ya watu wa Peponi?
Swali: Je, imethibiti kuwa kiarabu ndio lugha ya watu wa Peponi? Jibu: Ni jambo limetangaa. Udhahiri wa Hadiyth ni kwamba ndio lugha yao. Udhahiri wa Hadiyth zilizisimuliwa ni kwamba watawasiliana kwa kiarabu. Hata hivyo haikupokelewa katika Hadiyth Swahiyh kwamba watawasiliana kwa lugha ya kiarabu.
In "Pepo"
121. Nasaba ya Mtume ( صلى الله عليه وسلم) na aina mbili za waarabu
Kuhusu nasaba yake yeye ni Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Muttwalib bin Haashim bin ´Abdul-Manaaf bin Quswayy bin Kilaab. Anatokana na kabila la Quraysh ambalo ndio kabila bora. Quraysh wanatokana na kabila la Ismaa´iyl (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Waarabu wamegawanyika aina mbili kwa yaliyotangaa: 1- Waarabu wa asili (al-´Arab al-´Aaribah).…
In "Sharh Thalaathat-il-Usuwl – al-Fawzaan"