Swali: Vipi Ibraahiym atakuwa ni Muislamu ilihali Uislamu ulikuja baada yake?

Jibu: Wewe hujui ni nini Uislamu. Maana ya Uislamu ni kujisalimisha kwa Allaah kwa Tawhiyd (kumpwekesha), kunyenyekea Kwake kwa utiifu na kujitakasa na Shirki na kujitenga mbali na washirikina. Huu ndio Uislamu katika kila zama na mahala na ndio Uislamu ambao Allaah Amewatuma kwao Mitume wote. Kila Mtume na wafuasi wao walikuwa juu ya Uislamu. Kila yule ambaye alijisalimisha kwa Allaah na akamtii na akatendea kazi Shari´ah Yake katika ule wakati wake, basi huyo ni “Muislamu”. Hali iliendelea kuwa namna hii mpaka pale Alipotumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikawa “Uislamu” ni yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka hapo Qiyaamah kitaposimama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-08.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014