Mimi sio “´Allaamah” – mimi ni mwanafunzi mchanga!

Mwenye kufungua muhadhara:

Enyi ndugu! Hakika neema ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) juu yetu ni kubwa na fadhila Zake ni kuu. Miongoni mwa neema hizi kubwa ni kupatikana katika jamii yetu wanachuoni Rabbaaniyyuun. Ndevu zao zimekuwa nyeupe kwa kujifunza na kufunza. Kushukuru neema hii inakuwa kwa watu kupokea elimu yao na wafaidike na uzowefu wao. Katika usiku huu wenye baraka tunafarijika kwa kumkaribisha mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni wa jamii hii na Ummah huu wenye baraka. Naye si mwingine ni muheshimiwa na ´Allaamah Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy. Ni Ustadhw wa chuo kikuu cha Imaam Muhammad bin Suu´d. Atatueleza kuhusu maudhui kubwa kuhusu sababu za kuzidi na kupungua kwa imani. Tunamkaribisha.

ar-Raajhiy:

Ninamshukuru ndugu alotangulia mbele kwa maneno yake. Napenda kumjulisha ya kwamba mimi sio kama alivyonisifu kuwa ni “´Allaamah”. Hii ni sifa nisiyoistahiki. Mimi ni mwanafunzi mchanga na bado mpaka sasa nasoma. Hivyo sistahiki laqabu hii. Ninamuomba Allaah Anisamehe mimi na yeye na wasikilizaji. Ninamuomba Allaah Aturuzuku sote elimu yenye manufaa na matendo mema na Atuwafikishe kwa matendo mema yanayomridhisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 17/11/2014