Swali: Ninaomba nasaha kwa vijana juu ya kulazimiana na wanachuoni na khaswa katika wakati kama huu.

Jibu: Tunawanasihi wana wetu wanafunzi na ndugu zetu wengine walazimiane na elimu ya Kishari´ah na wachukue elimu kutoka kwenye vyanzo vyake; Qur-aan na Sunnah kupitia mikono ya wanachuoni waliobobea katika elimu, wanoajulikana kuwa na ´Aqiydah sahihi. Mtu asisemi kuwa anajua kusoma na kuandika. Sio kila mwenye kujua kusoma na kuandika anakuwa mwanafunzi. Kila mtu anajua kuandika na kusoma. Ni watu wangapi wana shahada ya udaktari ilihali ni wajinga wasiojijua? Anaitwa kuwa ni mjinga asiyejijua ilihali yuko na shahada ya udaktari. Leo elimu ya Kishari´ah imekuwa chache sana na wanachuoni wa Shari´ah ambao ni wajuzi juu ya Allaah na Dini yake wamekuwa wachache mno. Ujinga ndio umeenea na khaswa ikiwa mtu anatoka Saudi Arabia. Hata sisi vilevile tuna ujinga mwingi.

Nasaha yangu kwa ndugu zangu na wana wetu wanafunzi watumie fursa ya ujana na walazimiane na kutafuta elimu kwa njia zake mbali mbali. Leo njia za kutafuta elimu zimekuwa nyingi – himdi zote ni za Allaah.

Miongoni mwazo ni kusoma kwenye vyuo vikuu vya Kishari´ah.

Miongoni mwazo ni kuhudhuria mizunguko ya kielimu ambayo inafanywa Misikitini.

Miongoni mwazo ni kusikiliza kaseti za wanachuoni.

Miongoni mwazo ni kuwasiliana na wanachuoni na kuwauliza maswali.

Miongoni mwazo ni kusoma vitabu vya wanachuoni.

Leo darsa zinatolewa kwenye tovuti. Mtu anaweza kufuatilia darsa na yuko nyumbani mwake.

Salaf walikuwa wakipupia kutafuta elimu, wakitaabika, wakitumia juhudi kubwa na kujitahidi, wakisafiri kwenda kutafuta elimu na wakiwaacha wake zao na watoto wao kwa muda mrefu na wakikesha usiku.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 17/11/2014