Swali: Kuna mtu kila Ijumaa anatuma SMS ilio na Kauli ya Allaah (Subhaanah):

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah anamsifu Nabii. Na Malaika Wake pia [wanamuombea du’aa]. Enyi mlioamini mswalieni na msalimieni maamkizi ya amani.” (33:56)

Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kufanya ni maalum kutuma Aayah hii kila Ijumaa?

Jibu: Ni jambo limeamrishwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kila Ijumaa. Ni bora kufanya hivo Ijumaa kuliko siku zingine. Pamoja na hivyo ninaonelea kuwa si jambo la sawa kuwatumia watu kwa njia zote zinazowezekana. Kwa sababu wanaweza kufikiria kuwa ni jambo la wajibu kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015