Swalah ya mwanamke kwenye chumba cha hoteli Makkah

Swali: Swalah ya mwanamke kwenye chumba cha hoteli nje ya msikiti Mtakatifu ni bora kuliko katika msikiti Mtakatifu?

Jibu: Ndio. Huku ni kujisitiri zaidi. Kuswali kwake nyumbani ni kujisitiri zaidi. Ni bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah. Nyumba zao ni bora kwao.”

Hili linahusu misikiti yote, Makkah, al-Madiynah na kwenginepo.

Jambo lingine ni kwamba msikiti Mtakatifu haukukomeka karibu na Ka´bah peke yake. Misikiti yote Haram katika Makkah ni katika msikiti Mtakatifu. Himdi zote ni za Allaah. Ni pana. Msilifanye humu kwenu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015