Mwanafunzi asiyekuwa sawa na viatu vya wanachuoni

Swali: Kuna wanafunzi wanaosema kuwa haitakikani kuzingatia masharti ya Ijtihaad yaliyowekwa na wanachuoni. Kwa sababu Maswahabah na Taabi´uun hawakuwa na sifa hizi zinazotajwa…

Jibu: Walikuwa ni wanafunzi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawakuwa na vigezo hivi? Mtu anayechukua elimu moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuwa hana vigezo hivi? Ametakasika Allaah! Ni maneno ya kipumbavu! Hawana vigezo? Wanafunzi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Taabi´uun wamesoma kwa Maswahabah. Walikuwa wanafunzi wao. Hawakuwa na vigezo? Wewe si lolote ukilinganishwa na wao. Huna hata elimu ilio sawa na sandala zao. Vipi unaweza kuzungumza namna hii na kusema kuwa wanachuoni wana makosa?

Unayezungumza namna hii; wewe ni kama Imaam Abu Haniyfah, Imaam Maalik, Imaam ash-Shaafi´iy na Imaam Ahmad? Je, wewe ni kama wao? Hawa ndio Mujtahiduun kwa kuwa wana masharti ya Ijtihaad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015