Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya mashindano ya wasichana ya kusoma Qur-aan tukufu kwa utungo ipasavyo (ترتيل) na kwa kuwepo wanaume?

Jibu: Wasichana kusoma Qur-aan kwa utungo ipasavyo kwa kuwepo wanaume haijuzu. Kunachelea juu yao wakafitinishwa naye. Shari´ah imekuja kuziba njia zote zinazopelekea katika haramu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/127)
  • Imechapishwa: 22/08/2020