Inafaa kwa mwanamke kusoma kwa sauti ya juu?

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusoma kwa sauti ya juu katika swalah ya Subh, Maghrib na ´Ishaa kama mwanaume au yeye anatakiwa kusoma kwa sauti ya siri?

Jibu: Ikiwa yuko peke yake nyumbani, yuko na Mahram zake au yuko pamoja na wanawake wenzake tu anaweza kusoma kwa sauti ya juu. Akiwaongoza wanawake wenzake katika swalah nyumbani kwake na wako wao wenyewe tu anaweza pia kusoma kwa sauti ya juu.

Ama ikiwa anaswali na pembezoni mwake kuna wanaume ambao ni ajinabi kwake wanasikia sauti yake, bora zaidi asisome kwa sauti ya juu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (126/04)
  • Imechapishwa: 22/08/2020