Mlango: Njia nyingi za kheri
[Miongoni mwa njia za kheri] kuna ambao wanapenda kujifunza elimu. Elimu leo naweza kusema kuwa ni miongoni mwa matendo bora zaidi ya kimwili. Hakika watu leo wanahitaji elimu ya Shari’ah. Ujinga umekuwa mwingi na wanaojifanya kuwa ni wanachuoni wamekuwa wengi. Watu ambao wanadai kuwa ni wanachuoni ilihali ni wababaishaji tu. Hakika tuna haja ya kujifunza elimu. Mtu awe na elimu iliyobobea kabisa na imara. Elimu ambayo imejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah ili aweze kuraddi vurugu hizi ambazo zimeanza kuenea kila kona. Kila mtu ambaye amejifunza Hadiyth moja au mbili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) anajiweka kimbelembele kutoa fatwa na kuchukulia wepesi. Utafikiri yeye sasa ndio amekuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Imaam Ahmad, as-Shaafi´iy au maimamu wengineo. Hiki ni kielelezo chenye kuonyesha khatari ilio kubwa ikiwa Allaah hatouletea Ummah wanachuoni wakubwa walio na elimu iliyobobea na hoja zenye nguvu.
Kwa ajili hii ndio maana ninaonelea kuwa kutafuta elimu leo ndio tendo ambalo ni bora zaidi kwa viumbe. Kutafuta elimu ni bora zaidi kuliko swadaqah na Jihaad. Bali kutafuta elimu kwenyewe ni Jihaad. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amefanya kukaenda sambamba na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/149-150)
- Imechapishwa: 03/03/2024
Mlango: Njia nyingi za kheri
[Miongoni mwa njia za kheri] kuna ambao wanapenda kujifunza elimu. Elimu leo naweza kusema kuwa ni miongoni mwa matendo bora zaidi ya kimwili. Hakika watu leo wanahitaji elimu ya Shari’ah. Ujinga umekuwa mwingi na wanaojifanya kuwa ni wanachuoni wamekuwa wengi. Watu ambao wanadai kuwa ni wanachuoni ilihali ni wababaishaji tu. Hakika tuna haja ya kujifunza elimu. Mtu awe na elimu iliyobobea kabisa na imara. Elimu ambayo imejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah ili aweze kuraddi vurugu hizi ambazo zimeanza kuenea kila kona. Kila mtu ambaye amejifunza Hadiyth moja au mbili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) anajiweka kimbelembele kutoa fatwa na kuchukulia wepesi. Utafikiri yeye sasa ndio amekuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Imaam Ahmad, as-Shaafi´iy au maimamu wengineo. Hiki ni kielelezo chenye kuonyesha khatari ilio kubwa ikiwa Allaah hatouletea Ummah wanachuoni wakubwa walio na elimu iliyobobea na hoja zenye nguvu.
Kwa ajili hii ndio maana ninaonelea kuwa kutafuta elimu leo ndio tendo ambalo ni bora zaidi kwa viumbe. Kutafuta elimu ni bora zaidi kuliko swadaqah na Jihaad. Bali kutafuta elimu kwenyewe ni Jihaad. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amefanya kukaenda sambamba na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/149-150)
Imechapishwa: 03/03/2024
https://firqatunnajia.com/mashaykh-wenye-vilemba-vya-ukoka-wanaojifanya-ni-wanachuoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)