Mtu akimsengenya muislamu mwenzake Aakhirah atachukua katika matendo yake mema. Inasemekana katika Salaf kuna mtu aliambiwa “fulani anakusengenya.” Basi akamtengenezea zawadi kisha akamtumia nayo. Yule mtu aliyemsengenya akashangaa sana ni vipi atamsengenya kisha tena amtumie zawadi. Msengenywaji akamwambia nimefanya hivo kwa sababu na wewe umenizawadia kunipa mema yako ambayo hayapotei. Pamoja na kuwa mimi nimekuzawadia zawadi  ambayo itapotea papahapa duniani. Haya ni malipo kwa kunipa zawadi. Tazama Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) walivokuwa na uelewa.

Kwa kifupi tunachotaka kusema ni kuwa usengenyi ni haramu na ni katika madhambi makubwa na khaswakhaswa ikiwa inahusiana na kuwasengenya watawala na wanachuoni.Kuwasengenya watu hawa ni kubaya zaidi kuliko watu wengine. Kwa sababu kule kuwasengenya wanachuoni kunafanya watu kudharau ile elimu walioibeba na ambao wanawafunza watu. Matokeo yake watu hawakubali yale wanayowafunza, jambo ambalo linaidhuru dini. Na kuwasengenya watawala kunafanya watu kuwakosea heshima na kuwafanyia uasi, jambo ambalo mwisho wake linapelekea katika vurugu isiyosemekana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/121-122)
  • Imechapishwa: 03/03/2024