Swali 48: Ni ipi neno la haki kuhusu kusoma vitabu vilivyoandikwa na wazushi na kusikiliza kanda zao?

Jibu: Haijuzu kusoma vitabu vya wazushi na wala kusikiliza kanda zao isipokuwa kwa yule anayetaka kuwaraddi na kubainisha upotofu wao.

Ama mtu anayeanza, mwanafunzi, mtu wa kawaida au ambaye anasoma kwa ajili ya kusoma tu na si kwa lengo la kuraddi na kubainisha hali yake, huyu haifai kwake kuvisoma. Kwa sababu vinaweza kuuathiri moyo wake na vikambabaisha na hivyo akapatwa na shari yake[1].

[1] Kumepokelewa mapokezi mengi kutoka kwa Salaf yanayotahadharisha Ahl-ul-Ahwaa´ wal-Bid´ah. Hapa chini yanafuatia baadhi ya mapokezi…

Abu Qilaabah amesema kuhusu Ahl-ul-Bid´ah:

”Usikae nao na usichangyike nao. Hakika mimi nachelea wasikutumbukize ndani ya upotofu wao au wakakubabaisheni mambo katika yale mnayoyatambua.” (al-Laalakaa’iy (1/134), al-Bid´a wan-Nahiy ´anhaa (55) na al-I´tiswaam (1/172))

Ibraahiym an-Nakha´iy amesema:

”Usikae na wazushi na wala usizungumze nao. Kwani hakika mimi naogopa nyoyo zenu zisije kukengeuka.” (al-Bid´a wan-Nahiy ´anhaa (56) na al-I´tiswaam (1/172)

Abu Qilaabah amesema:

”Ee Ayyuub! Usiwaruhusu Ahl-ul-Ahwaa´ kukusikiliza.” (al-Laalakaa’iy (1/134))

al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

”Ukimuona mzushi kwenye njia basi chukua njia nyingine.” (al-Ibaanah (2/475))

Haafidhw Sa´iyd bin ´Amr al- Barda´iy amesema:

“Nilikuwa na Abu Zur’ah wakati alipoulizwa kuhusu al-Haarith al-Muhaasibiy na vitabu vyake. Akamjibu muulizaji: “Ninakutahadharisha na vitabu hivi. Vina Bid´ah na upotevu. Shikamana na mapokezi. Humo kuna yakutosheleza kwako.” Kukasemwa: “Kuna mafunzo ndani yake.” Akasema: “Asiyekuwa na mafunzo katika maandiko ya Allaah hana mafunzo yoyote katika vitabu hivi. Ni upesi ulioje watu kuingia ndani ya Bid´ah!” (at-Tahdhiyb (2/117) na Taariykh Baghdaad (8/215))

Imaam Ahmad alizungumza maneno makali juu ya al-Muhaasibiy pale aliposema:

”Usidanganyike na unyenyekevu na upole wake. Usidanganyike na kuinamisha kwake kichwa. Ni mtu muovu. Hakuna anayemtambua isipokuwa tu yule mwenye uzoefu naye! Usizungumze naye. Hatakiwi kuonyeshwa heshima. Je, wewe unakaa na kila mzushi anayesimulia Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hapana. Hatakiwi kuonyeshwa heshima!”  (Twabaaqaat-ul-Hanaabilah (1/233))

Huu ndio mfumo wa Salaf katika kutangamana na Ahl-ul-Bid´ah. Huo ndio ulikuwa msimamo wao juu ya vitabu na kusikiliza maneno yao. Vivyo hivyo ndivo kunaweza kusemwa juu ya kanda zao. Kufokafoka kwa maneno yao kwenye kanda kuna khatari zaidi. Je, vijana wetu wataufahamu mfumo huu na kujitenga mbali na vitabu na kanda za Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ katika zama zetu hizi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 135
  • Imechapishwa: 23/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy