47. Usahihi wa mfumo wa mtu unamuamulia kuingia Peponi au Motoni?

Swali 47: Usahihi wa mfumo wa mtu unamuamulia kuingia Peponi au Motoni?

Jibu: Ndio. Mfumo ukiwa sahihi basi mwenye nao anakuwa katika watu wa Peponi. Akiwa na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Salaf basi anakuwa ni katika watu wa Peponi kwa idhini ya Allaah. Na akiwa na mfumo wa wapotofu basi ni mwenye kutishiwa kuingia Motoni. Kwa hivyo mfumo, kusihi na kutosihi kwake, kunamuamulia mtu kuingia ima Peponi au Motoni[1].

[1] Anaingia chini ya utashi wa Allaah (Ta´ala). Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ikiwa mfuno si wenye kumuamulia mtu kuingia Peponi au Motoni, ni ipi faida ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

” Na Ummah wangu utagawanyika katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: ”Ni lipi hilo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Ni lile linalofuata yale ninayofuata mii hii leo na Maswahabah zangu.”?

Yule ambaye anafuata mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) basi huyo ni katika watu wa Peponi. Asiyekuwa hivo basi kuna khatari akaadhibiwa.

Ni jambo linalotambulika kwa mujibu wa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ya kwamba yale makundi sabini na mbili sio yenye kuwekwa Motoni milele. Hakuna yeyote katika Ahl-ul-Hadiyth aliyesema hivo, kwa hiyo yazingatie hayo! Isipokuwa ikiwa kama Bid´ah yake hiyo ni kufuru na kipote chake ni cha kikafiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 03/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy