Malaika ndani ya nyumba ya mtu mwenye janaba

Swali: Nyongeza aliyoipokea Abu Daawuud inayosema kuwa Malaika hawaingii ndani ya nyumba iliyo na mbwa, picha au mwenye janaba.

Jibu: Ni jambo linatakiwa kutazamwa vyema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akilala usiku hali ya kuwa na janaba. Anatosheka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wudhuu´ wa swalah na akilala ilihali yuko na janaba. Ingelikuwa Malaika wanajizuilia kutokana na mtu mwenye janaba basi asingelilala (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa na janaba kwa sababu kipindi hicho anaweza kuteremshiwa wahy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22815/هل-صح-ان-الملاىكة-لا-تدخل-بيتا-فيه-جنب
  • Imechapishwa: 26/08/2023