Mwenye janaba hasogelewi na Malaika?

Swali: Mtu ambaye ameota na kumwaga hasogelewi na Malaika?

Jibu: Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipojiliwa na Abu Hurayrah na Hudhayfah na wakajaribu kumkwepa, akasema:

“Hakika muislamu hanajisiki.”

Janaba ni maana katika maana na sio najisi. Ni maana katika maana inayowajibisha josho. Vivyo hivyo hedhi inawajibisha josho. Lakini mwanamke anabaki kuwa ni msafi kukiwemo jasho lake, mate yake, kile anachokigusa ni kisafi na nywele zake ni safi. Kadhalika mwenye janaba ni msafi kukiwemo jasho lake na mwili wake ni msafi. Hata hivyo ni lazima kuoga kama alivyoamrishwa na Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22814/ما-صحة-ان-المحتلم-لا-تقربه-الملاىكة
  • Imechapishwa: 26/08/2023