Makatazo ya kunywa kutoka kwenye mdomo wa kiriba au chupa

Swali: Malengo ya kukatazwa kunywa moja kwa moja kutoka kwenye mdomo wa kiriba ni ili kusitoke ndani kitu cha kumdhuru?

Jibu: Udhahiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni ili kusitoke kitu chenye kumdhuru.

Swali: Vipi ikiwa ni kutoka kwenye chupa linaloonyesha ndani kuna nini?

Jibu: Muhimu ni kwamba sio haramu. Inachukiza. Kwa ajili hiyo alikunywa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwenye mdomo wa kiriba wakati kulipokuwa na haja ya kufanya hivo. Lakini ikiwa inawezekana kunywa kutoka kwenye chombo ndio salama zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23263/حكم-وحكمة-النهي-عن-الشرب-من-فم-القربة
  • Imechapishwa: 14/12/2023