337 – Abu Tha´labah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Alikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa vita vya kushambulia Khaybar, ambapo wakapata ndani ya bustani yake vitunguu maji, vitunguu saumu na figili. Wakaanza kuvila kwa sababu walikuwa na njaa. Wakati watu walipoenda msikitini basi msikiti ukaanza kutoa harufu ya kitunguu maji na kitunguu saumu, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

مَنْ أكل من هذه الشجرة الخبيثة فلا يقرّبنا

“Anayekula kutoka kwenye mti huu mbaya basi asitukurubie.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy kwa cheni ya wapokezi nzuri.

338 – Kwa Muslim imepokelewa takriban namna hiyo kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, hata hivyo hakukutajwa kitunguu maji[2].

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/256)
  • Imechapishwa: 14/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy