Swalah ndio mafungamano yaliyo kati ya mja na Mola Wake. Swalah ndio nguzo yenye nguvu kabisa baada ya Shahaadah. Swalah ndio yenye kupambanua baina ya muislamu na kafiri. Swalah ndio ahadi ilio kati yetu waislamu na washirikina na makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliyopo baina yetu na wao ni swalah. Hivyo basi, mwenye kuiacha amekufuru.”[1]

bi maana amekufuru kufuru yenye kumtoa katika Uislamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliyopo baina yetu na wao ni swalah.”

Swalah ndio yenye kupambanua kati ya waislamu na makafiri.

[1]at-Tirmidhiy (2621)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/303)
  • Imechapishwa: 02/05/2023