23. Mfano wa vichenguzi vya Uislamu III

Mfano mwingine akapinga kitu kinachotambulika vyema katika dini na wakati huohuo ni mtambuzi na anakusudia; na si mjinga au mwenye kupindisha maana. Kwa mfano mtu huyo anapinga uharamu wa uzinzi, ribaa, uharamu wa kunywa pombe, uharamu wa kushuhudia uwongo, uharamu wa kuwaasi wazazi wawili, kuwakata ndugu, uharamu wa kula mali ya yatima, au anapinga maelezo aliyoeleza Allaah au hukumu moja wapo ya kiislamu inayotambulika vyema, au anapinga ulazima wa kumwabudu Allaah, anapinga sifa na majina ya Allaah, kitu katika mambo ya dharurah ya dini, anapinga ulazima wa kumwabudu Allaah (Ta´ala), kumpwekesha, kumtii, anapinga ulazima wa kuswali, ulazima wa kutoa zakaah, ulazima wa kufunga Ramadhaan, ulazima wa kuhiji Nyumba ya Allaah kwa mwenye uwezo au akaacha swalah kwa uvivu na uzembe hata kama hakupinga ulazima wake. Mtu aina hii ni kafiri kwa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Imaam Muslim amepokea kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika baina ya mtu na baina ya shirki na kufuru ni kuacha swalah.”[1]

Ahmad na watunzi wa Sunan wamepokea kupitia kwa Buraydah bin al-Haswiyb (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ

“Wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.”[3]

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ

“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[4]

Swalah, amani na baraka zimwedee mja na Mtume Wake Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

[1] Muslim (82).

[2] at-Tirmidhiy (2621) ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh na geni.”

an-Nasaa´iy (463), Ibn Maajah (1079) na Ahmad (22937).

[3] 09:11

[4] 09:05

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 29-31
  • Imechapishwa: 02/05/2023