Mwenye kuacha swalah ni kafiri kinyume na mtu mwenye kuacha kufunga Ramadhaan na akawa anakula na kunywa mchana wa Ramadhaan na hajali. Huyu hatusemi kuwa ni kafiri. Lakini lau ataacha swalah ni kafiri. Akikusanya pesa na akawa hatoi zakaah, hatusemi kuwa ni kafiri. Lakini lau ataacha swalah tunasema kuwa ni kafiri. Akiacha kwenda kuhiji pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya hivo, hatusemi kuwa ni kafiri. Lakini lau ataacha swalah tunasema kuwa ni kafiri. ´Abdullaah bin Shaqiyq (Rahimahu Allaah), ambaye ni mmoja katika wanafunzi wa Maswahabah na ni mtu anayejulikana, amesema:

“Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna kitu katika matendo walichokuwa wakionelea kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah tu.”[1]

Hivyo basi, swalah ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiamrisha lau mtu ataiacha ni kama mfano wa kuacha Tawhiyd. Mwenye kuacha swalah anakuwa kafiri mshirikina – tunaomba kinga kwa Allaah.

[1]at-Tirmidhiy (2622)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/304)
  • Imechapishwa: 02/05/2023