Madalali wanaowasaidia wafanya biashara wenye kula ribaa

Swali: Je, inamgusa pia laana yule ambaye anatangamana na wala ribaa?

Jibu: Anaingia ndani ya maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

”… na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[1]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewatahadharisha waja Wake kutokana na kusaidiana katika dhambi na uadui kukiwemo ribaa, wizi, ujambazi, kufanya ghushi katika miamala na kila kinachowadhuru watu. Na ambaye anawasaidia katika ribaa na kuwaletea ile bidhaa wanayojisaidia kwayo katika ribaa zao kunakhofiwa juu yake jambo hili. Haijalishi kitu hata kama yeye hakula, lakini kunakhofiwa juu yake. Kwa sababu thamani anazochukua kutoka kwao zinaingia katika chakuka chake.

[1] 05:02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23431/هل-يدخل-في-اللعن-من-يتعاون-مع-اهل-الربا
  • Imechapishwa: 19/01/2024